Unknown Unknown Author
Title: GARETH BALE: RONALDO NI MWANASOKA NA MTU SAFI!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
GARETH BALE amesisitiza Mchezaji mwenzake wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, ni Mtu mwema sana tofauti na baadhi ya Watu wanavyomchuku...
BALE_IN_REALGARETH BALE amesisitiza Mchezaji mwenzake wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, ni Mtu mwema sana tofauti na baadhi ya Watu wanavyomchukulia.BALE_N_RONALDO13
Bale alijiunga Real Madrid akitokea Tottenham Mwaka Jana kwa Dau la Euro Milioni 100 likipiku Dau la Ronaldo aliponunuliwa toka Man United la Euro Milioni 94.
Hata hivyo, Bale, Raia wa Wales, amesisitiza Ronaldo alimkaribisha vyema Jijini Madrid na ametamka: “Tangu nifike hapa amekuwa Mtu wa ajabu kwa kunisaidia ndani na nje ya Uwanja. Ni Mtu mwema, anasaidia sana, na Siku zote anataka Timu ishinde lakini Watu wanaandika tofauti!”
Bale pia amekiri Luka Modric, ambae walikuwa nae Tottenham na kuhamia Real Mwaka mmoja kabla, amekuwa mkarimu sana kwake.
Bale ameeleza: “Tulikuwa na Luka Miaka mitano Spurs na tulikuwa na uhusiano mzuri sana na hili limenisaidia nilipokuja hapa. Yeye alitua hapa hamjuia Mtu na ilikuwa ngumu kwake. Lakini nilipokuja mimi nimemkuta yeye na nilifarijika sana.”
Bale pia amesema kuwepo kwa Watu maarufu kama kina Zinedine Zidane, ambae yupo chini ya Meneja wa Real Madrid, Carlo Ancelotti, kumemwinua sana.
Mbali ya kuisaidia Real Madrid kutwaa Copa del Rey Msimu huu baada ya kufunga Bao la Pili, la ushindi na la ajabu dhidi ya Barcelona Mwezi uliopita, Bale pia ana nafasi kubwa hapo Mei 24 kutwaa Ubingwa wa Ulaya wakati Real Madrid itakapokutana na Atletico Madrid huko Lisbon, Ureno kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIOZ LIGI.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top