Kuna wanamuziki ambao wamejipatia umaarufu mkubwa kupitia tasnia ya muziki, kwa kuufanya uvutie ndani na nje ya nchi.
Vile vile
wanamuziki hao wamedumu kwenye tasnia hiyo kwa zaidi ya miaka 40,
miongoni mwa wanamuziki hao ni pamoja na Hamza Kalala, ambaye amewahi
kupewa majina kadhaa kama vile mzee wa Madongo na Komandoo.
Historia ya Kalala kwa ufupi
Alizaliwa mkoani Tanga na kusoma shule za msingi na sekondari mkoani humo.(Martha Magessa)
Baba yake
Komando alikuwa mfanyakazi wa Shirika la Reli, katika Stesheni ya
Mpanda, ambaye baadaye alihamishiwa mkoani Tanga ambako alibahatika kuoa
mke wa kabila la Kizigua, ambaye ndiye mama wa Komando Kalala.
Mara baada ya Komando kuzaliwa alipewa jina la 'Kapesula,' akiwa ni mchanganyiko 'chotara' wa makabila ya Kinyamwezi na Kizigua.
Komando
Kalala alianza kuhamasika katika mambo ya muziki mwaka 1966 akiwa darasa
la nne, wakati alipokuwa akimshuhudia baba yake akiimba na kucheza
ngoma ya Kinyamwezi ya 'Manyanga' ambayo ilitokana na ngoma ya 'Hiyari
ya Moyo', huko huko Tanga.
Wakati
huo wakata mkonge walikuwa wakifanya mashindano ya ngoma kati ya
Wanyamwezi na ngoma za makabila mengine waliokuwa katika mashamba
tofauti ya mkonge ya Kibaranga, Amboni na mengine mengi.
Lakini
ngoma ya 'Manyanga' ya Wanyamwezi na ile ya 'Sindimba' ya Wamakonde
ndizo zilizokuwa zikitia fora katika mashindano hayo kila mara. Kalala
anaeleza, hakufundishwa muziki na mtu bali ni kutokana na ngoma hizo
alizokuwa akicheza na kuimba baba yake, na kumuiga kupiga gitaa mjomba
wake ambaye alikuwa na gitaa nyumbani.
Anasema
alipima uwezo wake wa muziki alipokuwa kwenye bendi zilizokuwapo kwenye
mashamba ya Mkonge kama Kwanduru Jazz Band, na Amboni Jazz.
Hakuvutiwa
na maisha ya mashambani hivyo alirudi Tanga Mjini, ambako aliendelea na
mazoezi ya kupiga gitaa nyumbani kwao, siku moja alipita Mkongo mmoja
aliyekuwa akijulikana kwa jina moja la Chivosha, akavutiwa kwa jinsi
alivyokuwa akipiga gitaa na kumuomba ajiunge na bendi yao ya Villa Negro
Successes.
Anasimulia
huku kote alikuwa anatoroka na baba yake hakuwahi kufahamu kama
anaimba, alichelea kumwambia kwa kuogopa kukatishwa tamaa.
CHANZO:MWANANCHI
Post a Comment